Baraka FM
Baraka FM
24 May 2025, 20:52

Wataalamu wa afya watakiwa kutoa kipaumbele kwa vijana katika kuwapa elimu ya afya ili kuwasaidia kuondokana na changamoto zinazochangiwa na ukosefu wa elimu hiyo.
Na Lukia Chasanika
Shirika la DSW Tanzania limeendelea kutoa elimu mbalimbali kwa vijana waliopo vyuoni na nje ya mfumo rasmi wa shule ikiwemo afya ya akili, stadi za maisha na afya ya uzazi kwa vijana.
Akizungumza katika tamasha la michezo liliwakutamisha vijana wa vyuo mbalimbali vilivyopo mkoani Mbeya mgeni rasmi ambaye ni mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya daktari Maisara Kame amelishukru shirika la DSW Tanzania kwa kulichagua kundi la vijana vyuoni kutoa elimu ya afya ya akili na uzazi.

Kwa upande wake daktari wa magonjwa bingwa ya akina mama na mhadhiri wa chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Judica Christopher amesema kijana ana haki ya kupata huduma za afya bila kuulizwa maswali ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi salama na mpango wa uzazi.

Aidha daktari wa afya ya akili kutoka hospitali ya mkoa wa Mbeya Mbeya Daktari Reinfridy Chombo amesema dalili za kutambua kama mtu ana tatizo la afya ya akili ni kujitenga na wenzake ,kuwa mtu wa huzuni wakati pamoja na kutaka kujidhuru yeye mwenyewe pamoja na watu waliokaribu yake.
Naye Konsolata Mung’ong’o kutoka jeshi la polisi kitengo cha ukatili wa kijinsia mkoa wa Mbeya amesema vijana wanatakiwa kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi wakiwa shuleni na vyuoni kwani moja ya changamoto amabyo inawakumba vijana wengi kuathirika kisaikolojia baada ya mahusiano kuvunjika.
Mratibu wa mradi wa SAFA kutoka shirika la DSW Tanzania mkoa wa Mbeya Mariam Ibrahim amewashukru viongozi na wataalam mmbalimbali wanaoendelea kushirikiana nao kutoa elimu wa vijana vyuoni na katika jamii.
Mmoja wa vijana walioshiriki katika michezo wa liaza na kukimbiza kukua Esther Mbogo amesema elimu inayotolewa na wadau mbalimbali kupitia shirika la DSW Tanzania katika mabonza ya michezo iwe endelevu kwa vijana ili iwasaidia wanapokuwa vyuoni.
