Baraka FM
Baraka FM
19 May 2025, 17:53

Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuwahimiza wakristo kuendelea kuombea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu ili uweze kufanyika kwa amani na wapatikane viongozi wenye maono.
Kufuatia tukio kubwa la uchaguzi wa viongozi mbalimbali ndani ya taifa letu mwaka huu 2025 Askofu Robert Pangani amewahimiza viongozi wa dini kuwahamasisha wakristo kuomba juu ya tukio hilo,na viongozi wa kanisa kwa ujumla
Na Deus Mellah
Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi Mch Robert Pangani wakati akizungumza na waumini katika ibada ya maombi ya kuliombea taifa na kanisa hilo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mchungaji Sevilwe Msyaliha amesema kazi ya kanisa ni kuombea viongozi wake na taifa kwa ujumla.

Naye katibu idara ya uwakili jimbo Mchungaji Paul Mwambalaswa amesema maombi hayo yatakuwa yanafanyika mara kwa mara katika sehemu mbalimbali ndani ya kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi.
Baadhi ya waumini kutoka madhehebu mbalimbali wameshiriki katika maombi hayo na kuupongeza uongozi wa kanisa la moravian jimbo la kusini magharibi chini ya Askofu Robart Pangani
