Baraka FM
Baraka FM
10 May 2025, 07:31

Zao la pareto ni miongoni mwa mazao ya biashara yanayolimwa nchini Tanzania,katika Mikoa ya Mbeya zao hili limekuwa likilimwa katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya,Rungwe,Busokelo na katika mkoa wa Songwe zao hili linalimwa katika wilaya ya Ileje.
Na Hobokela Lwinga
Serikali kupitia taasisi ya utafititi wa mbegu Tanzania TARI UYOLE imewahahakishia wakulima wa zao la pareto kupata mbegu bora zitakazowapa tija ya uzalisha wa Uhakika wa zao Hilo.
Hayo yamesemwa na mtafiti wa zao la pareto kutoka taasisi ya utafititi wa mbegu TARI UYOLE Rachel Ndala wakati akizungumza katika Semina ya mawakala wa kampuni ya ununuzi wa pareto Tanzania PCT katika ukumbi dkt.Tulia wa chama cha mapinduzi Mbeya mjini.
Bi.Rachel amesema wanashirikiana vizuri na kampuni ya PCT hivyo wakulima wachangamkie ulimaji wa zao hilo kwani soko lake ni kubwa ukilinganisha na mazao mengine.

Kwa upande wake mhasibu Mkuu wa PCT Gerard Joseph amewahakikishia wakulima kununua zao hilo zaidi ya tani 2000 kwa bei nzuri hivyo amewataka wakulima kuzalisha maua yenye ubora kwani zao hilo linavunwa kwa misimu yote ya kilimo.

Aidha afisa Pareto katika mikoa ya Mbeya na Songwe kupitia PCT Musa Malubalo amesema ili kuendelea kuwawezesha wakulima kupata tija wamejipanga kutoa vikaushio vipya zaidi ya 100 ili wakulima waweze kukausha pareto kwa ubora.

Baadhi ya wakulima walioshiriki semina hiyo wamesema pareto ni zao ambalo limewapa mafanikio makubwa tunau ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto wao,kujenga nyumba sambamba na kuongeza uchumi wa familia zao.
