Baraka FM
Baraka FM
8 May 2025, 19:20

Zao la kahawa ni miongoni mwa mazao ya biashara yenye mchango mkubwa Katika kuongeza kipato kwa mtu na taifa.
Na mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Dkt. Juma Z. Homera amezindua Mradi wa kuendeleza mnyororo wa thamani endelevu wa kahawa Tanzania utakaogharimu takribani Dola za Marekani 337,171 kwa Kipindi Cha Miaka mitatu.
Akiwa katika Ukumbi wa Eden Jijini Mbeya Dkt.Homera amesema Mradi huu utatekelezwa katika vyama Tisa vya Msingi(AMCOS) vilivyochaguliwa Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na Rungwe Mkoani Mbeya na Wilaya ya mbinga Mkoani Ruvuma.

Katika Miaka mitatu(2025-2028) Mradi huu unatarajiwa kuwafikia Wakulima 1359 Kutoka katika vyama vya Msingi(AMCOS) Ameongeza Dkt. Homera na Kutoa wito kwa Wawekezaji nchini Japan kuwekeza katika zao la mpunga linalolimwa Wilaya ya Mbarali.
Akieleza malengo ya Mradi huu Balozi wa Japan nchini Tanzania Mikai Yoachi amesema Lengo kubwa ni kubadilisha Kilimo Cha wazalishaji wadogo kwa njia endelevu kwa kuboresha uzalishaji wao na upatikanaji wa Soko kwa kuchochea ushiriki wa sekta binafsi na Uwekezaji katika Kilimo na mifumo ya Chakula.

Katika Kikao hicho mbali na Uwepo wa Balozi wa Japan nchini Tanzania kimeweka bayana kuwa Shirika la Cafe Africa Tanzania, ndio Mtekelezaji Mkuu na Kampuni za UCC na Marubeni Kutoka nchini Japan.