Baraka FM
Baraka FM
8 May 2025, 19:10

Jukumu la kuzuia vitendo vya rushwa katika jamii ni suala la kila mtu kwani rushwa imekuwa ni adui wa haki na kusababisha kukwama kwa maendeleo.
Na Hobokela Lwinga
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Mbeya TAKUKURU imefanikiwa kuokoa shilingi milioni 15 kutoka katika kikundi cha YOUTH REVOLUTION GROUP zilizotokana na mikopo ya asilimia kumi ya halmashauri iliyotolewa katika halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa mbeya Maghela Ndimbo wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi yake kuhusu mafanikio ya utendaji kazi kwa miezi mitatu january – machi 2025.

Aidha Ndimbo amesema wamefanikiwa kurejesha eneo la ekari nne kwa mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi zilizouzwa kinyume na taratibu,sheria na miongozo ya uendeshaji wa mamlaka.

Katika hatua nyingine mkuu huyo Amewataka wananchi kutoa taarifa za rushwa kuelekea kipindi cha uchaguzi october,2025 pindi wanapoona kwenye maeneo yao huku akisema taasisi yake inaendelea kutoa elimu juu ya athari za rushwa.