Baraka FM
Baraka FM
30 April 2025, 10:35

Kutokana na umuhimu wa afya jamii inahimizwa kuipa kipaumbele sekta hiyo kwa kupima afya zao mara kwa mara.
Na Deus Mellah
katika kuadhimisha wiki ya wataalam wa maabala katika hospitali ya rufaa kanda ya mbeya wananchi mkoani mbeya wametakiwa kushiriki katika tukio hilo kwa kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali bure.
Akizungumza na kituo hikii mkuuwa huduma za maabala katika hospitali hiyo DR Frank Kimalo amesema katika kuadhimisha wiki hiyo wanafanya huduma za vipimo mbalimbali vya afya na kutoa elimu kwa wananchi wanaofika kupata huduma katika eneo hilo.
DR Frank Kimalo amesema ni mhimu wananchi kujitokeza kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kwa manufaa yao.

Naye afisa mteknolojia wa maabala na afsa ubora wa maabala Isack Nyangi amesema wamekuwa wakitoa ushauli wa kimaabala kwa wananchi wanaoendelea kufanya vipimo katika hospital hiyo.

Nao baadhi ya wanachi walio fanya vipimo katika eneo hilo wamewaomba madaktari hao kufanya huduma hizo kuwa endelevu ili wananchi wengi wapate fursa YA kupata huduma hiyo.