Baraka FM
Baraka FM
27 April 2025, 13:15

Kanisa la Mungu linapaswa kuwa na mazingira Mazuri ya kumwabudia Mungu kwani kufanya hivyo kunafanya kazi yake isongee mbele.
Na Mboka Mjafula
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Saza wilaya ya Songwe mkoani Songwe unaongozwa na mchungaji Enerd Mwashibale limefanya ibada ya kuweka jiwe la msingi nyumba mpya ya kuabudia.
Katika ibada Hiyo imeongozwa na kamati tendaji iliyowakilishwa na Makamu mwenyekiti wa Jimbo mchungaji Asulumenye Mwahalende.

Wageni wengine walioshiriki ibada hiyo ni Pamoja na mwenyekiti wa kanisa la Moravian wilaya ya Chunya mchungaji Anyandwile Kajange.

Sambamba na hiyo kwaya mbalimbali zimehudhuria zikiwemo za ndani na nje ya ushirika Pamoja na wageni wengine.
Endelea kutusikiliza na kutufuatilia Kupitia redio Baraka 107.7Mhz tuko live na kwa matukio mengine tufuatilie kupitia mitandao ya kijamii Facebook na Instagram kwa jina la@barakafmradio na online https://radiotadio.co.tz/barakafm