Baraka FM

Wanafunzi washauriwa kutokutumia uzazi wa mpango

27 April 2025, 13:04

Baadhi ya wanafunzi ambao wameshiriki mkutano huo wa UKWATA Chunya Mbeya

Kutokana na uwepo njia tofautitofauti za uzazi wa mpango wanafunzi wanao endelea na masomo ngazi ya Sekondari wameshauriwa kuto kutumia njia hizo mpaka watakapo ingia katika ndoa

Na Hobokela Lwinga

Kutokana na matumizi holela ya dawa za uzazi wa mpango,Wanafunzi wa shule za secondary nchini wametakiwa kuepuka na kuachana na tabia ya kutumia uzazi wa mpango kabla ya kuingia kwenye ndoa.

‎Rai hiyo imetolewa na nesi Muunguzi katika zahanati ya Luwalaje Winnie Changani wakati akiwafundisha somo la afya wanafunzi walioshiriki mkutano wa pasaka (Easter conference) mkoa wa chunya ki Ukwata iliyofanyika katika shule ya Sekondari lupa  iliyopo halmashauri ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Muunguzi katika zahanati ya Luwalaje Winnie (picha na Hobokela Lwinga)

Katika hatua nyingine ameelezea madhara ya kutumia uzazi wa mpango kabla ya ndoa ni kupata uvimbe kwenye uzazi, kuharibika kwa homoni pamoja na kupata utasa.

‎Kwa upande wake mwalimu Lwimiko Kabuje ambaye ni mlezi wa UKWATA mkoa wa Chunya Amesema wanafunzi wengi wanaingia na kuharibu ya afya zao kutokana na utandawazi huku akieleza kuwa katika kutambua hilo kumekuwa na hatua mbalimbali za kutoa elimu ya afya ya uzazi.

Baadhi ya wanafunzi walio shiriki mkutano huo(picha na Hobokela Lwinga)

Aidha Mkuu wa chuo cha Biblia cha Utengule kinachomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Philimoni Andrew Nyilenda ameomba elimu hiyo ya afya eendelee kutolewa kwa wananchi wengi kwani ni muhimu kwa kizazi cha sasa na cha badae.

Mkuu wa chuo cha Biblia cha Utengule cha kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch. Philimoni Andrew Nyilenda

‎Baadhi ya wanafunzi ambao wameshiriki mkutano huo wa UKWATA wameomba kuwe na mwendelezo katika utoaji elimu ya afya ya uzazi ili waweze kuelewa na kukabiliana na vichocheo vinavyoharibu maisha yao.