Baraka FM
Baraka FM
23 April 2025, 18:24

Kutokana na changamoto ya watu wengi kukumbwa na tatizo la macho,KKKT Dayosisi ya Konde wameandaa kambi ya madaktari bingwa watakao toa matibabu kwa wiki moja bure mkoani Mbeya.
Na Ezra Mwilwa
Askofu Geofrey Mwakihaba wa kanisa la KKKT dayosisi ya konde amewataka wakristo na watu wote wanyanda za juu kusini kushiriki katika uzinduzi wa hospital mpya ya kibigwa itakayo ambatana na marathon yenye lengo la kusaidia watu wenye matatizo ya macho mkoani Mbeya.
Askofu Mwakihaba amesema hayo katika uzinduzi wa marathoni hiyo ambapo ameeleza kuwa fedha zitakazopatikana zitaelekezwa katika ununuzi wa vifaa tiba na kugharamia matibabu kwa watu wenye changamoto ya macho itayotolewa na madaktari bingwa kutoka hospital ya KCMC.

Aidha askofu Mwakihaba amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu kila anayetamani kutia nia asitumie rushwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya na udiakonia Daktari Lee Mmwakalinga amesoma risala mbele ya Askofu akieleza maomba mbalimbli kutoka Idara hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya marathon Angumbwikye Mwalupogo amesema katika kipindi cha kambi ya madaktari bingwa Kila mwenye changamoto ya macho ajitokeze kupata matibabu hayo.

Nao baadhi ya wakisto wamesema watu wa Mbeya watumie fursa hii kupata tiba.
