Baraka FM
Baraka FM
19 April 2025, 13:19

Dunia ina mambo kila inapaoitwa leo matukio ya mauaji yamezidi kuongezeka.
Na Ezekiel Kamanga
Mchungaji Golden Ngumbuke(66)wa Kanisa la Pentecoast Evengelical Fellowship Africa(PEFA)la Iganzo Jijini Mbeya ameuawa nje ya nyumba yake Mtaa wa Mwafute Kata ya Ilemi na wananchi waliojichukulia sheria mkononi wakituhumu kumuua jirani yake kwa ushirikina Katekista Fadhili Komba(32)wa Kigango cha Mwasenkwa Parokia ya Mwanjelwa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya.
Kaimu Mtendaji wa Kata ya Ilemi Herman Mbanga amesema suala hilo lilijadiliwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mtaani hapo ambapo ilidaiwa kuwepo mgogoro wa mpaka baina ya majirani hao pia Katekista kudaiwa mchungaji kumpiga mke wa mchungaji ambapo mchungaji alishindwa kesi ndipo alipomtamkia Katekista kuwa yeye si mchungaji wa kawaida na kutakiwa kumuomba radhi jambo ambalo Katekista alitekeleza na kwenda kutoa sadaka kanisani.

Pamoja na kutekeleza maagizo ya mchungaji katekista alianza kuumwa ugonjwa wa kuhara tangu mwezi Desemba mwaka jana hadi umauti ulipomkuta April 15, 2025.
Siku chache baada ya kifo cha Katekista watu wasiojulikana walivunja vioo vya dirisha na banda la bata ndiyo mchungaji Ngumbuke alipiga picha na kuzua tafrani kwa vijana ambao walimshambulia mchungaji nje ya nyumba yake mpaka kupoteza maisha.
Polisi waliuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi na baadhi ya wananchi wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo.
Chifu George Lyoto amesema wananchi waache tabia za kujichulia sheria mkononi ilhali akionya kuachana na vitendo vya ushirikina ingawa Serikali haiamini ushirika.

Aidha Katibu wa ulinzi Kata ya Ilemi Tosha Nundu amekiri kulishughulikia suala hilo na kwamba walizuia mchungaji kuwepo hapo lakini walishangazwa na kitendo cha mchungaji kurejea eneo hilo.
Mazishi ya mchungaji yatafanyika Aprili 19,2025 nyumbani kwao mtaa wa Sistila Kata ya Iyunga Jijini Mbeya ilhali juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya kuthibitisha tukio hilo na idadi ya watu wanaoshikiliwa mpaka sasa kwa tuhuma za mauaji.