Baraka FM

Zaidi ya wakulima 25,000 kunufaika na maonesho ya wakulima Festival 2025 Mbeya

17 April 2025, 19:19

Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Dynamic agriculture program akizungumza na wanahabari Mkoani Mbeya (picha na Hobokela Lwinga).

Kilimo ni uti wa mgongo,maelfu dunia ya watu duniani wamefanikiwa kufanya maendeleo mbalimbali kupitia kilimo.

Na Hobokela Lwinga

Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na taasisi isiyoya kiserikali ya Dynamic agriculture program Mbeya imeanza maonesho ya kilimo yajulikanayo kama wakulima Festival 2025.

‎Akizungumzia maonesho hayo Mkurugenzi wa taasisi ya Dyanamic agriculture program Fadhili Alson Swillah amesema maonesho hayo yatajumuisha watu Zaidi ya 25,000 na itajumuisha kata tisa za halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Sauti yaMkurugenzi wa taasisi ya Dyanamic agriculture program Fadhili Alson Swillah

‎Katika hatua nyingine baadhi ya wawakilishi wa makampuni ambayo yatashiriki maonesho hayo wamesema watakuwa na bidha mbalimbali ambazo zinamchango mkubwa katika kuwezesha kilimo bora kwa wakulima.

Sauti za baadhi ya wawakilishi wa makampuni ambayo yatashiriki maonesho

‎Aidha meneja wa taasisi ya kifedha ya Azania bank Bw Samson mahimbi amesema katika kuwawezesha wakulima ipo account ya wakulima ambayo inatoa fursa ya kupata mikopo ya kilimo yenye riba nafuu.

Sauti yameneja wa taasisi ya kifedha ya Azania bank Bw Samson mahimbi

‎Maonesho hayo yatafanyika kuanzia April 25-30,2025 katika Kijiji cha Jojo kata ya santilya tarafa ya isangati halmashauri wilaya Mbeya yenye taswira ya kuongeza tija kwa wakulima.