

26 March 2025, 17:32
Katika kuhakikisha urahisi wa utendaji kazi shughuli za kikanisa, kanisa la Moravian wilaya ya Mbalizi wamefanya harambee ya ununuzi wa Gari
Na Hobokela Lwinga
Viongozi wa Kanisa la Moraviani Tanzania wilaya ya Mbalizi wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa ueledi na ufanisi ili kuhakikisha kanisa linapiga hatua kubwa kimaendeleo.
Hayo yamesemwa na Askofu wa kanisa hilo Mch. Robert Pangani wakati wa ibada ya harambee kwa ajili ya ununuzi wa gari iliyofanyika kanisa la Moraviani ushirika wa Yeriko na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.
Askofu Pangani amesema fedha zote zilizokusanywa kupitia harambee hiyo zielekezwe kwenye lengo lililokusudiwa na kwamba hivi sasa kanisa linataka kuongeza magari kwa ajili ya ofisi ya katibu mkuu.
Hata hivyo Mwenyekiti wa wilaya ya mbalizi kanisa la Moravian mchungaji Erica Samwanijembe amewashukuru watu wote waliofanikisha zoezi la uchangiaji.
Zaidi ya shilingi milioni thelathini zimepatikana katika harambee ya ununuzi wa gari ya kanisa la Moravian wilaya ya Mbalizi.