

25 March 2025, 21:59
Kifo ni fumbo wengi tuliozungumza nao na kuishi nao hawapo wamelala,hii ni safari ya kila mmoja wetu katika ulimwengu huu ulioumbwa na Mungu.
Na Hobokela Lwinga
Katibu wa umoja wa vijana wa zamani kanisa la Moravian Andrew Wilmas Seleman Mwankenja amefariki dunia.
Mzee Mwankenja ni miongoni mwa wakristo wakongwe waliolitumikia kanisa kwa muda mrefu ambapo mpaka mauti inamfika alikuwa katibu wa idara ya kwaya ya umoja wa vijana wa zamani yenye makao makuu yake katika kanisa la Moravian ushirika wa mabatini Mbeya.
Nje na kanisa Mzee Mwankenja amekitumikia chama chama cha mapinduzi katika wadhifa wa katibu wa chama hicho mkoa wa Mbeya.
Ibada ya mazishi itafanyika alhamisi machi 27,2025 katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Meta na kisha kuzikwa Katika makaburi ya Iwambi jijini Mbeya.
Mzee Andrew Wilmas Seleman Mwankenja alizaliwa mwaka 1968 na amefariki machi 25,2025.