

25 March 2025, 07:24
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amesema ni jambo ambalo haiwezekani Chama hicho kupata matokeo ya uchaguzi wa asilimia sifuri kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwaka 2024 katika mkoa wa Mbeya na maeneo mengine hivyo kueleza kuwa ni vigumu kuishinda CCM bila mabadiliko ya sheria za uchaguzi
Na Josea Sinkala
Lissu amesema hayo katika uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya kwenye mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa operesheni ya No reforms no election.
Amesema haiwezekani kuindoa CCM madarakani kwasababu mfumo uliopo wa uchaguzi ni wa chama hicho tawala (CCM).”Kwa mfumo huo wa CCM ndio maana wagombea wetu wanaenguliwa, hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi eti kutoka kuongoza jijini la Mbeya na kuwa na Mbunge ambaye aliongoza kwa kura katika nchi nzima bwana Sugu sasa lazima tubadilishe utaratibu wa uchaguzi.
Mambo yanayotakiwa kubadilishwa wanayafahamu tangu enzi za jaji Nyarali, weka tume huru, hakikisha kura feki haziingizwi na Polisi na walimu wanaosimamia uchaguzi na ndio maana tunasema jukumu letu la kwanza ni mapambano ya kubadilisha utaratibu huu wa uchaguzi na yakitushinda hayo tumekwisha”, ameeleza Tundu Lissu, mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Aidha amesema ili kubadilisha mfumo huo wa uchaguzi ni kukwamisha uchaguzi huo Katika mikutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho na aliyewahi kuwa mgombea Urais (CHADEMA) Dr. Wilbroad Slaa amerejea CHADEMA na kupokelewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa TunduALissu.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA jijini Mbeya kwenye uzinduzi wa operesheni hiyo ya No reforms no election, iliyozinduliwa katika kanda ya Nyasa, amewaomba radhi wana CHADEMA na wananchi kwa kukosana kwa kipindi fulani lakini ameamua kurudi CHADEMA kwasababu ni wapigania haki wakisimama na kampeni yao ya no reform no election Dr. Slaa ameahidi kushirikiana na CHADEMA kupigania haki na mabadiliko ya kweli.
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA (Tanzania bara) John Heche, amesema Tanzania ina utajiri mwingi lakini watu wake ni fukara kutokana na uongozi mbovu Serikalini.
Heche amewaomba wananchi kushikama kuhakikisha Serikali inaongoza upatikanaji wa katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na marekebisho ya sheria za uchaguzi ili kupata viongozi wanaowataka kwa maendeleo yao akisema CHADEMA ndio chama mbadala katika kuwatumikia wananchi.
Viongozi wengine mbalimbali wamehutubia katika mkutano huo akiwemo mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu), katibu mkuu wa BAWACHA Taifa Pamela Maasai, mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Taifa Rose Mayemba, mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya Masaga Pius Kaloli na wengineo wengi ambapo baada ya uzinduzi huo mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu ameelekea katika mikoa ya Rukwa na Songwe huku makamu mwenyekiti bara John Heche akielekea katika wilaya za Kyela na Mbarali, mkoa wa Njombe kisha kuhitimisha kwa pamoja mkoani Iringa ambapo agenda mama ni kuelimisha wananchi juu ya kampeni yao ya No reforms no election inayolenga kushinikiza upatikanaji wa mifumo na sheria rafiki za kiuchaguzi.