Baraka FM

Mch. Nzowa awataka waumini kuishi maisha ya toba

23 March 2025, 12:10

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi mchungaji Lawrence Nzowa

Kila mwaka wakristo duniani wamekuwa na mwezi maalumu wa mfungo ambao hukadiliwa kwa March-April kabla ya sikukuu ya pasaka,mwezi ambao umekuwa na msisitizo wa kutenda na kufanya matendo ya huruma kwa watu mbalimbali ikiwemo makundi maalumu.

Na Hobokela Lwinga

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi mchungaji Lawrence Nzowa amewataka waumini na watu wote kuutumia mwezi wa kwaresma kuishi maisha ya Toba.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook mchungaji Nzowa amesema mwezi wa kwaresma kila mtu anapaswa kuishi maisha mema ikiwa ni pamoja na kuwatumikia wengine.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameomba katika mwezi huu Mungu ajalie kuyaweza hayo.

“Wakati wa Kwaresma,Mungu atuwezeshe tuyaishi maisha ya Toba daima tukiwatumikia wengine (wafilipi 2:3). Yehova Mungu atujalie site”.

Ikumbukwe kuwa wakristo wote duniani wameanza mwezi wa kwaresma machi 05,2025 hii ikiwa ni kuelekea katika maadhimisho ya sikukuu ya pasaka April 20,2025.