Baraka FM

USCF Cuom yafanya ibada, Ambwene ahudumia mamia ya vijana Mbeya

23 March 2025, 10:50

Mtumishi wa Mungu Ambwene Mwasongwe akiendelea huduma ya maombi kwa vijana katika KKKT Usharika wa Forest jijini Mbeya

Maandiko 1 Yohana 2:14Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

Na Hobokela Lwinga

Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT Kupitia umoja wa wanafunzi vyuo vikuu tawi la mzumbe( USCF Cuom) wamefanya ibada kubwa ya mkesha jijini Mbeya iliyowakutanisa mamia ya vijana.

Baadhi ya vijana wakiwa katika ibada ya mkesha KKKT Usharika wa Forest jijini Mbeya

Vijana hao wamefanya ibada hiyo machi 21,2025 katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania dayosis ya Konde usharika wa Forest karibu na Bank kuu ya Tanzania jijini Mbeya.

Katika ibada hiyo mtumishi wa Mungu mwimbaji wa nyimbo za injili na mwalimu wa neno la Mungu Ambwene Mwasongwe amehudmu.

Mwimbaji wa nyimbo za injili na mwalimu wa neno la Mungu Ambwene Mwasongwe akifundisha katika ibada hiyo

Watumishi wengine walishiriki katika ibada na kuhudumu ni pamoja Joshua Godfrey kiongozi wa USCF Cuom, Mchungaji mwenjeji Benedictor Mwaijande na mlezi wa tawi mchungaji Whisper Siwiti.

Joshua Godfrey kiongozi wa USCF Cuom

Ikumbukwe wanafunzi hao wamekuwa na nyakati tofauti tofauti za kumtumikia Mungu ikiwa ni pamoja na kuandaa ibada za kusifu na kuabudu.