Baraka FM

Askofu Pangani aongoza mamia kumzika Maria Kajinga

23 March 2025, 10:01

Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Robert Pangani(katikati )akiweka shada kaburini (kushoto)ni Askofu mstaafu Lusekelo Mwakafwila(kulia) ni Askofu Kenani Panja wa Jimbo la kusini

Hakuna mtu ajuaye siku ya kufa kwake hivyo tunapaswa kujiandaa kwa maisha mema ya kimwili na Kiroho.

Na Hobokela Lwinga

Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Robert Pangani ameongoza mamia ya waombolezaji katika msiba wa Maria Kajinga mama mzazi wa mwenyekiti wa kanisa hilo wilaya ya Mbeya mchungaji Osia Mbotwa.

Katika ibada ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Forest mpya wageni wengine walioshiriki ni pamoja na Askofu Kenani Panja wa Jimbo la kusini na Askofu mstaafu Lusekelo Mwakafwila wa jimbo Hilo.

Marehemu Maria Kajinga enzi za uhai wake

Aidha katika ibada hiyo viongozi wengine waliohudhuria ni Makamu mwenyekiti na Kaimu Katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Asulumenye Mwahalende na viongozi wengine halmashauri kuu ya jimbo.

Ikumbukwe Marehemu Maria Kajinga amefariki machi 20,2025 na amezikwa machi 23,2025 katika jiji la Mbeya.

Msafara wa waombolezaji ukielekea kanisani