

21 March 2025, 22:08
Serikali inapotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yetu jamii inapaswa kuwa walinzi ili kuondoa uharibifu unaoweza kujitokeza.
Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mh,Halima Mdee amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbarak Alhaji Batenga kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhalibifu wa miundombinu ya Umeme katika Shule ya msingi Amani uliofanywa na takribani Miezi 13 Nyuma na kupelekea baadhi ya Fedha kubadilishwa matumizi kinyume na miongozo ya OR-TAMISEMI.
Mdee ametoa Rai hiyo baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Tamimu Kambona Kutoa Ufafanuzi wa kwanini Kichomea taka kimejengwa Chini ya kiwango ilihali Fedha za kutosha zililetwa.
Katika Majibu yake Kambona amesema Fedha ya kichomea taka ililetwa lakini Kiasi kadhaa kilichukuliwa na kukarabati miundombinu ya Umeme ambayo iliibiwa katika Shule hiyo na licha ya kesi kufunguliwa lakini bado mwafaka haujapatikana na ni takribani Miezi 13 mpaka sasa.
“Kuchukuliwa kwa Kiasi hicho Cha Fedha kwaajiri ya miundombinu katika Ile iliyotengwa kujenga kichomea taka ndiyo sababu imepelekea kijengwe chini ya kiwango maana Fedha yake ilikuwa haitoshi”Amesema Kambona.
Mdee ameyasema hayo Leo March 21 Wilayani Chunya wakati akiongoza Wajumbe wa Kamati hiyo Kukagua na kupokea Taarifa ya matumizi ya Fedha katika Utekelezaji wa Miradi mitatau ikiwemo Jengo la Halmashauri, Nyumba ya Mkurugenzi, na Ujenzi wa Shule ya msingi Amani iliyoko Kata ya Makongolosi.
Aidha amesema si Vema Halmashauri kufurahia hoja za kiukakuzi kwa kuwa asili ya hoja hizo hujitokeza pale wahusika wanapokiuka Taratibu na miongozo ya matumizi ya Fedha kwa mujibu wa Sheria, badala yake wajikite katika ufanyaji Kazi mzuri utakaoondoa hoja za kiukakuzi.
Wajumbe wa Kamati wametoa Maelekezo kwa Halmashauri ya Chunya kuhakikisha kabla ya Tarehe 31 Disemba 2025 kichomea taka kiwe kimejengwa upya kwa mjibu wa ramani na miongozo ya OR-TAMISEMI na Taarifa ya ukamilishwaji iwasilishwe kwa CAG kabla ya January 10,2026