

21 March 2025, 12:55
Mapema Leo katika jiji la Mbeya hari imekuwa si shwari katika barabara mlima nyoka baada ya magari matatu kugongana.
Na Hobokela Lwinga
Watu kadhaa wamenusurika kifo kufuatia ajali ya basi la New Force liliokuwa linatokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa basi la new force limegongana na Malori matatu maeneo ya Mlima Nyoka jijini Mbeya.
Katika ajali hiyo baadhi ya abiria wamepata majeraha madogo madogo.
Juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya zinaendelea ili aweze kuthibisha tukio hilo.Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi.