

18 March 2025, 19:38
Kuelekea uchaguzi Mkuu October 2025 vyama mbalimbali vya siasa vimeanza kutambiana na kutoa kauli mbalimbali
Na Hobokela Lwinga
Makamu Mwenyekti Wa Chama Cha Mapinduzi (Ccm) Stephen Wasira, Amesisitiza Kuwa Hakuna Mtu Yoyote Ambaye Anaweza Kuzuia Uchaguzi Mkuu Mwaka Huu Usifanyike.
Akizungumza Na Wananchi Jijini Mbeya Katika Ziara Yake Mkoani Humo, Wasira Amewahakikishia Watanzania Kuwa Uchaguzi Mkuu Unaotarajia Kufanyika Oktoba Mwaka Huu Uko Pale Pale Na Hakuna Mtu Yoyote Anayaweza Kuuzuia.
Wasira Amesisitiza Kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Baada Ya Kuingia Madarakani Amekuja Na R Nne Ikiwemo R Inayowakilisha Maridhiano Ambayo Yamewezeasha Hata Waliokuwa Wamekimbia Nchi Kurejea Nchini Na Wako Salama.
Wasira anaendelea na ziara yake mkoani humo, ambapo Leo ametembelea halmshauri ya wilaya ya rungwe, na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali.