

15 March 2025, 18:18
Kifo kifo hakichagui mtu, safari hiyo kila mtu ni lazima aipitie kwa wakati wake na kwa njia yake.
Na Hobokela Lwinga, Mbeya
Aliyekuwa mke wa mchungaji marehemu Kalengo Salome Magwaza amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Kanda ya Mbeya.
Akitoa taarifa ya msiba huo, Makamu mwenyekiti na Kaimu Katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Asulemenye mwahalende amesema marehemu amefariki machi 14,2025.
Aidha katika taarifa ya mchungaji Mwahalende amesema marehemu Salome Magwaza ataagwa jumapiili machi 16,2025 majira ya saa kumi kamili alasiri katika ushirika wa Nzovwe Moravian na atazikwa jumatatu machi 17,2025 katika kijiji cha Matula-Mbozi mkoani Songwe.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa kifo cha mama mchungaji Salome Magwaza kimetokana na ajali aliyoipata wiki mbili nyuma.