

11 March 2025, 21:03
Kutokana uwepo vyama mbalimbli vya mikopo Naibu waziri wa Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka viongozi na wanachama wa chama kuongoza vya hivyo kwa weledi.
Na Ezekiel Kamanga
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka viongozi na wanachama wa Chama Cha Akiba na mikopo Lulu Saccos kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na weredi kwa kusimamia misingi ya sheria kanuni nataratibu walizojiwekea ili kupunguza malalamiko na migogoro ya mara kwa mara.
Mahundi amesisitiza kwa viongozi wa Chama hicho kuendelea kuwa waadilifu kutunza mali na fedha za Lulu Saccos ili kuboresha huduma katika Chama chao na kuhakikisha mikutano ya wanachama inafanyika kwa uwazi ili kujadili taarifa husika.
Mhandisi Mahundi amezungumza hayo mara baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa wiki ya maadhimisho ya Chama Cha Akiba na Mikopo cha Lulu Saccos Ltd unaofanyika Jijini Mbeya ukilenga kuwajengea uwezo wanachama sanjari na kupanga namna ya kutoa sadaka pia misaada mbalimbali kwa vituo vya watoto yatima,wazee wasiojiweza na wenye mahitaji.
“Kwa hiyo kukaa hapa siku tatu kupatiwa elimu hizi zote namna ambavyo zimepangwa na bodi yetu mimi ninakiona hiki Chama kinakuwa bora zaidi kwa sababu watu wameelimika na hivyo mtafanya vizuri na hata wale wachache waliokuwa wanalegalega kupitia elimu ya siku tatu naamini tutakwenda kufanya vizuri zaidi katika maeneo yote”alisema Mhandisi Mahundi.
Mahundi amesema Chama hicho kinahitaji pongezi kwani uwekezaji uliopo umekuwa na tija hadi kufika mtaji wa bilioni kumi na saba kutoka milioni kumi na tatu walizoanza nazo hatua ambayo itasaidia kuongeza na kukuza mtaji walionao.
Amesema kuwa maendeleo ya Lulu Saccos hayawezi kuwa endelevu kama wanachama wanaokopa hawawezikurejesha kwa wakati ili kuweza kufanya vizuri kadri ya ulipaji wenu.
Nasisitiza mambo kadhaa katika mkutano wenu “matokeo ya mafunzo mtakayopewa katika maadhimisho ya wiki ya Lulu Saccos kwa mwaka 2025 yakaongeze uwekezaji zaidi katika Chama chenu ili mkawe mfano katika vyama vingine vya ushirika Akiba na Mikopo vilivyopo hapa nchini Tanzania”Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho Obeid Mtweve amesema chanzo cha mafanikio ya Lulu Saccos ni uaminfu katika urejeshaji wa mikopo na imani kwa viongozi wao kama bodi inavyotekeleza dhamana waliopewa kwa vitendo na kutoa taarifa zao kwa uwazi.
Amesema Lulu hawatafuti wanachama kiholela mwanachama lazima adhaminiwe na wanachama watatu ndani ya Lulu na kuchunguzwa mwenendo wake ndio maana Lulu imekuwa na msingi imara bila kuwa na migogoro ya kifedha kwa kufuata sera ya serikali iliyoelekeza kupitia ushirika ndio msingi imara wa uendeshaji.
Aidha mpaka sasa Chama hicho kina wanachama 499 ambao ndio wamekuwa wakopaji wa kati na wakubwa licha ya baadhi kushindwa kurejesha kwa wakati mara wanapokopa lakini ni wachache wambao wamekuwa wakishughulikiwa na chama hicho.
Amesema wakati mwingine baadhi yao wamekuwa wakishindwa kurejesha na kukimbilia mahakamani lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na uimara wa mwnasheria walieye naye kama Chama huku wengine wakipoteza sifa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kukosa uaminifu.
Chama Cha Akiba na Mikopo cha Lulu Saccos kinamiliki jengo lake la ghorofa lililopo Soweto Jijini Mbeya.