Baraka FM

Baada ya kushinda kesi, CHAKAMWATA yarejea upya na msimamo wa kikokotoo

6 March 2025, 18:13

Mwenyekiti wa chama cha CHAKAMWATA Taifa (katikati) picha na Hobokela Lwinga

Mwalimu ni mtu anayesaidia wengine kupata ujuzi, maarifa na tunu ambapo kazi hiyo inaweza kufanywa na yeyote katika nafasi maalum, mfano mzazi au ndugu akimfundisha mtoto nyumbani, lakini kwa wengine ndio njia ya kupata riziki inayomdai karibu kila siku kwa miaka mingi mfano shuleni.

Na Hobokela Lwinga

Baada ya miaka 6 na mwezi mmoja wa Chama Cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) kufungiwa, imeelezwa kuwa sasa kimerejea tena kwa lengo la kuendelea kutetea maslahi ya walimu nchini.

Baadhi ya viongozi wa chama cha CHAKAMWATA wakizungumza na wananabari mkoani Mbeya (Picha na Hobokela Lwinga)

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Mbeya, Mwenyekiti wa chama hicho nchini Mwalimu Ipyana Jackson Kabuje amesema chama kimepitia changamoto nyingi ikiwemo kupelekwa mahakamani, na kwamba wanaingia kwenye mapambano.

Mwalimu Kabuje ameongeza kuwa kwa sasa hawatakubali haki yao kupokwa na mtu yeyote yule kwa sababu kazi yao kubwa ni kuhakikisha haki ya walimu inapatikana katika nyanja zote ikiwemo masuala ya kiuchumi.

Sauti ya Mwenyekiti wa chama hicho nchini Mwalimu Ipyana Jackson Kabuje

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Haki na Maslai ya Walimu Tanzania (Chakamwata) Mwalimu Meshack Lupakisyo Kapange amesema kwamba wamerudi na Watanzania pale walipoishia, akisema wanaamini serikali ni sikivu hivyo itawapa ushirikiano mzuri.

Katibu Mkuu wa CHAKAMWATA Mwalimu Meshack Lupakisyo Kapange (katikati) Picha na Hobokela Lwinga
Sauti ya Katibu Mkuu wa Chakamwata Mwalimu Meshack Lupakisyo Kapange

Ikumbukwe kuwa Chakamwata ilikuwa kwenye kifungo tangu Februari 08 mwaka 2020 hadi Febuari 27, mwaka huu.