Baraka FM

Mhandisi Maryprisca akabidhi mabati bweni la wasichana Shizuvi

5 March 2025, 17:51

Mhandisi Maryprisca Mahundi akikabidhi mabati kwaajili ya ujenzi wa Bweni(picha na Hobokela Lwinga)

Naibu waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi atimiza Hadi yake kusaidia ujenzi wa Bweni

Na Hobokela Lwinga

Siku chache baada ya Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kuahidi mabati kwa ajili ya Bweni la Wasichana Shizuvi machi 4,2025 Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametekeleza ahadi yake kwa kukabidhi mabati yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili.

Baada ya kukabidhi bati hizo mhandisi Mahindi akiwa na viongozi wa UWT(picha na Hobokela Lwinga)

Akiwa Mgeni rasmi katika harambee ya changizo la ujenzi wa bweni lililojengwa kwa nguvu ya wananchi Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi aliahidi kuchangia ili kuwanusuru Wasichana kutembea umbali mrefu sanjari na kukatiza masomo kwa mimba zisizotarajiwa.

Akipokea mabati hayo katika ofisi za CCM Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi Diwani wa Kata ya Shizuvi Noah Mwashibanda amemshukuru Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kutekeleza ahadi yake kwa kipindi kifupi.

Diwani wa Kata ya Shizuvi Noah Mwashibanda akipokea msaada wa mabati hayo(picha na Hobokela Lwinga)

Afisa elimu Kata ya Shizuvi Joel Gabriel amesema kukamilika kwa Bweni hilo kutachochea ufaulu kwa watoto wa kike.

Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mbeya Subira Mwangoka kipekee amemshukuru Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kutafsiri Ubunge wake kwa vitendo kwa kuwajali watoto wa kike.

Aidha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya Akim Mwalupindi amesema Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi anatekeleza ilani kwa vitendo na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.