

3 March 2025, 10:29
Wakati majeruhi wa ajali iliyotokea eneo la shamwengo Mbeya wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya kanda Mbeya wageni mbalimbali mashuhuri wanafika kuwajulia hali.
Na Ezekiel Kamanga
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewatembelea majeruhi wa ajali iliyohusisha basi la CRN na Gari la miundombinu ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya iliyosababisha vifo vya watu wanne na majeruhi watano.
Miongoni mwa majeruhi waliotembelewa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ni pamoja na Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya Lucia Sule, Waandishi wa Habari Epmacus Kalokola,Denis George na Seleman Ndelage.
Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amepongeza uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa namna wanavyopana kuokoa maisha ya majeruhi huku akipongeza Serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan ilivyowekeza vifaa tiba hivyo kuokoa gharama kubwa kwenda hospitali nje ya Mkoa na nje ya nchi.
Wakati ikitokea ajali hiyo Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi alikuwa ziara ya kikazi nchini Zimbabwe.