Baraka FM

Miili ya waliofariki ajalini yaagwa Mbeya

27 February 2025, 20:04

Picha ikionyesha waandishi wa Habari wa kimuaga mwandishi aliye poteza maisha (picha Ezra Mwilwa)

Mkoa wa Mbeya kushirikiana na chama cha mapinduzi wameshiriki kuaga miwili ya watu wa nne(4) walio fariki.

Na Ezra Mwilwa

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella, leo tarehe 27 Februari 2025 ameongoza shughuli ya kuaga miili ya marehemu wanne waliopoteza maisha katika ajali ya gari wakati wakitokea kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhili Maganya, mkoani Mbeya.

Akiwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Mongella amesema chama kimetoa ubani wa shilingi milioni 20 kwa familia za marehemu na shilingi milioni 6 kwa majeruhi sita wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini ambaye pia ni Rais wa mbunge Duniani Dk Tulia Akson akiwasilisha salami za Rais (picha na Ezra Mwilwa)

Mongella ametoa pole kwa familia za marehemu na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.

Miwili ya marehemu ikiagwa na viongozi mbalimbli pamoja na wananchi(picha na Ezra Mwilwa(

Shughuli ya kuaga miili ya marehemu hao imefanyika katika Viwanja vya Soko la Uhindini, jijini Mbeya.