

26 February 2025, 08:47
Matumizi mabaya na kutokufuata sheria za barabarani kumegharimu maisha ya wengi wasio na hatia,uzembe huu umekuwa ukisababishwa na madereva wasiotii alama za barabarani.
Na Hobokela Lwinga
Watu watatu wamefariki dunia akiwemo mwandishi wa habari wa kujitegemea mkoani Mbeya Furaha Simchimba na wengine saba kujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea mkoani humo ikihusisha basi kampuni ya CRN na gari la serikali STM.
Ajali hiyo imetokea leo Februari 25 katika eneo la Shamwengo wilayani Mbeya wakati basi lenye namba T 599 DZQ likilipita gari la serikali lenye namba 6167 bila kuchukua tahadhari na kugongana nje ya barabara na kusababisha vifo hivyo na majeruhi saba akiwemo mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Mbeya, Epimacus Apolinary, Mwenyekiti na katibu wa UWT mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Mbeya Nebart msokwa amesema taratibu za kumpumzisha zinaendelea kwa kushirikiana na familia.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Wilbert Siwa amethibitisha ajali hiyo akieleza kuwa kati ya majeruhi saba wawili kati yao wapo mahututi.