

24 February 2025, 18:18
Wananchi Mbeya wafurahia ujio wa msaada wa kisheria wa mama Samia legal aid uliozinduliwa February 24,2025.
Na Hobokela Lwinga
Msaada Wa Kisheria Kwa Maana Ya Legal Aid imezinduliwa Mkoani Mbeya ikiwa Ni Na lengo la Kutatua Changamoto za Kisheria ambazo zinawakabili wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi, ndoa,ukatili wa Kijinsia na mengineyo.
Akizungumza katika uzinduzi wakampeni hiyo akiwa mgeni rasmi,Katika viwanja vya Stendi Ya Kabwe Jijini Mbeya,Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amesema amesema kwamba kampeni hiyo imekuja kwa dhumuni la kuwapatia elimu wananchi Pamoja na uelewa wa masuala ya kisheria na haki za binadamu.
Kwa upande wake katibu mkuu wa wizara ya Katiba na sheria Eliakimu Chacha Maswi amesema msaada huo wa kisheria utasaidia pia kuondokana na vitendo vya rusha huku akisema kwa mkoa wa Mbeya kampeni hiyo itatolewa kwa siku 15.
Akimwakilisha Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na makundi maalumu naibu katibu mkuu wa wizara hiyo Amon Mpanju amesema makundi yote yanayoshughulikiwa kwenye kampeni hiyo yanaratibiwa na wizara hiyo, akisistiza kila mmoja kuwajibika ili kukomesha vitendo vya kikatili katika jamii.
Nae mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge amesema migogoro mingi Mbeya inasababishwa na watendaji katika sekta ya sheria wasio waadilifu.
Aidha Akizungumza kwa niaba ya chama cha wana Sheria nchini TLS Baraka Mbwilo amewasihi mawakili na wadau wengine walioko kwenye tumu ya kutoa msaada wa kisheria kujitoa kwa moyo kuwasaidia wananchi kwa kutatua migogoro inayowakabili.
Akitoa salamu za Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia, wanawake na makundi maalumu Amon Mpanju (naibu katibu mkuu) amesema makundi yote yanayoshughulikiwa kwenye kampeni hiyo yanaratibiwa na wizara hiyo, akisema migogoro iliyopo instokana na maisha wanayoishi watanzani akisisitiza Kila mmoja kuwajibika vyema ili kukomesha vitendo vya ukatili kwenye jamii.
Nao baadhi ya wananchi mkoani humo wameishukru serikali kwa kutoa msaada huo wa kisheria Bure huku wakiomba uwe endelevu.
Uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama samia legal aid imebeba kauli mbiu isemayo “msaada wa kisheria , kwa haki usawa wa amani na maendeleo.