

13 February 2025, 13:42
Kulingana na mchango wa vyombo vya habari katika maendeleo ya nchi,TCRA imewakutanisha wadau kujadili na kujifunza mambo mbalimbali kuelekea uchaguzi Mkuu 2025.
Na Charles Amlike,Dodoma
Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na michezo Prof.Paramagamba Kabudi amevitaka vyombo vya habari viache kubananga lugha ya kiswahili badala yake vitumie misamiati sahihi ya lugha hiyo.
Waziri kabudi ameyasema hayo wakati akifungua mkutano Mkuu wa vyombo vya habari leo tarehe 13 Februari, 2025 dunia ikiwa inaadhimisha siku ya vyombo vya habari duniani katika ukumbi wa new generation jijini Dodoma unapofanyika Mkutano Mkuu wa wadau wa vyombo vya habari uliandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Dkt. Jabiri Kuwe Bakari amevitaka vyombo vya habari kuwa na utaratibu wa utunzaji wa Takwimu.
Katika hatua nyingine Msemaji Mkuu wa serikali na katibu Mkuu wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo Gerson Msigwa, ameishukuru na kuipongeza TCRA kwa kuwa na Jukwaa la kuwakutanisha wadau wa sekta ya habari pamoja.
Mkutano huo unakwenda na kauli mbiu isemayo wajibu wa vyombo vya habari kuelekea uchaguzi Mkuu 2025