Baraka FM

Mtoto wa miaka sita afa baada ya kutumbukia kwenye shimo la maji,Mbeya

8 February 2025, 06:31

Uangalizi kwa watoto ni muhimu sana ili kuwaepusha na majanga na hatari ambazo zinaweza kuwaepusha na hatari.

Na Hobokela Lwinga

Mtoto Aliyefahamika Kwa Jina La Vicent Konga Mwenye Umri Wa Miaka 6 Aliyekuwa Akisoma Darasa La Kwanza Katika Shule Ya Msingi Lyoto Iliyopo Jijini Mbeya Amefariki Dunia Baada Ya Kutumbukia Kwenye Korongo La Maji Lililopo Mtaa Wa Mwafute Kata Ya Ilemi Jijini Humo.

Akizungumzia tukio hilo Constable Alpha Isaya Afisa Habari Msaidizi wa Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji Mkoa Wa Mbeya amewataka wazazi na walezi mkoani humo kuwa walinzi wa watoto wao, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwaepusha na majanga mbalimbali ikiwemo ya vifo vitokanavyo na maji.

Aidha baadhi ya majirani wamesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tukio hilo,huku wakisema limekuwa funzo kwa kuwa Karibu Na Watoto wao ili kuwaepusha na majanga kama hayo.

Kwa mujibu wa balozi wa mtaa huo Lusekelo Mwaigabule amesema alipata taarifa za Kupotea kwa mtoto huyo siku ya jumatatu January 03,2025 jioni ndipo wakaungana na wananchi wake kwa ajili ya kumtafuta huku akisema siku ya jumanne walifanikiwa kumpata akiwa tayari amefariki katika korongo hilo lenye maji.