Baraka FM

Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya yaanza kutoa matibabu ya saratani

4 February 2025, 18:44

Haya ni maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Saratani duniani yaliyofanyika jijini Mbeya.

Katika kuboresha na kutoa huduma bora katika sekta ya afya serikali imeendelea kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amezindua wiki ya saratani Duniani maadhimisho yaliyofanyika Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya (MZRH).

Katika hotuba yake Malisa amewashukuru Madaktari wa Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kwa kutoa huduma bora huku akiwataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupima Ili kupata matibabu mapema kwa usahihi.

Aidha amewataka wataalamu kuendelea kutoa elimu kwa jamii Ili kutomeza ugonjwa wa saratani kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa”Tunaunganishwa kwa upekee wetu”.

Pia Beno Malisa ameiomba Hospitali kutoa motisha kwa watumishi wa Kitengo cha saratani kutokana na kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa kwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera

Lengo la kufanya maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa jamii sanjari na kuwahimiza kufika Hospitali kwa ajili ya kupata vipimo na matibabu kwani saratani inatibika.

Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya (MZRH)imezidi kupanua wigo katika huduma zake ambapo sasa ina Kitengo cha saratani kinachoongozwa na Dkt Irene Nguma.

Kwa upande wake Dkt Irene Nguma amesema Kitengo chake kwa sasa kimeimarika kwani awali huduma hizo zilikuwa zikipatikana Ocean Road pekee hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kupata vipimo na matibabu.

Risala imesomwa na Daktari bingwa wa saratani Dkt Tibera Rugambwa amesema kuna aina mbalimbali za saratani ikiwemo ya shingo ya uzazi,damu,mifupa na watoto ambapo sasa ni Kitengo hicho kimetoa huduma kwa miaka minne sasa.

Kama watoa huduma ni kuunganisha nguvu ili kugundua saratani kwa hatua za awali na kupata matibabu mapema.

“Mgonjwa wa saratani anahitaji upendo kama wagonjwa wengine “alisema Dkt Tibera Rugambwa.

Katika risala hiyo inaonesha Hospitali imekuwa ikipokea wagonjwa mia tano kwa mwezi hali inayoonesha ukubwa wa tatizo.

Daktari bingwa wa saratani Dkt Tibera Rugambwa kutoka hospitali ya rufaa Kanda ya Mbeya

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya Dkt Godlove Mbwanji ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maboresho ya idara ya saratani.

Dkt Mbwanji amesema saratani inatibika ambapo saratani ya shingo ya uzazi inaongoza kwa kusababisha vifo vingi kwa wanawake.

Amesema kukata tamaa na hofu kunasababisha vifo kwa wagonjwa zaidi wanadamu wanapaswa kumshukuru Mungu hata waamkapo kila leo na kupata nguvu mpya ya kufanya kazi.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya Dkt Godlove Mbwanji

Saratani inapitia hatua tatu ikiwemo ya dawa, upasuaji na mionzi na hivi karibuni huduma ya mionzi itapatikana Mbeya na kuisaidia Mikoa saba ya nyanda za juu.

Msagama Edmund Mpoto ni mmoja wa mashujaa wa saratani ameishukuru Serikali kwa kuisogeza huduma Mkoani Mbeya kwani imewapunguzia gharama wagonjwa.

Mpoto amesema wagonjwa wa saratani wamekuwa wakipokewa vizuri na kupata matibabu stahiki kutoka kwa watumishi wa Hospitali Kitengo kinachowapa faraja.

Mwalimu Varellia Mtega shujaa wa saratani ambaye mwaka 2000 aligundulika kuwa na ugonjwa wa saratani amewaatoa hofu wananchi kuwa ugonjwa wa saratani unatibika.

Mtega amewataka wananchi kujitokeza kupima na pia kuikubali hali hiyo huku akiishukuru Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kwa kuongeza kitengo cha saratani kwani kimewapunguzia gharama za safari ya kwenda Dar es Salaam.