

4 February 2025, 17:56
Mkoa wa Mbeya ni moja wapo ya mikoa ambayo inatekeleza zoezi la utoaji mikopo ya asilimia kumi kupitia halmashauri zake.
Na Hobokela Lwinga
Hamashauri ya Wilaya ya Chunya imekabidhi hundi ya Million 803,200,000 kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu ikiwa ni asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri ili kutimiza adhima ya serikali ya kuwezesha wananchi wake kujikwamua kiuchumi na kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Hundi hiyo imekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Alhaji Batenga leo wakati wa hafla ya utoaji mikopo kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na Watu wenyeu ulemavu kwa awamu ya kwanza iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya(Sapanjo).
Mkuu wa divisheni ya Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi Marietha Mlozi akisoma taarifa ya mikopo ya 10 % ya mapato ya ndani ya Halmashauri amesema kuwa jumla ya Vikundi 83 vitanifaika na Shilingi Millioni 803, 200,000 ambapo vikundi vya wanawake 41, Vijana 38 na Watu wenye ulemevu vikundi 4 ambavyo vimejikita katika shughuli tofauti tofauti.