

4 February 2025, 17:37
Duniani hatuna mji udumuo mataraijio yetu ni kuurithi ufalme wa milele wa Mungu ndio maana Mungu anatoa na kutwaa.
Na Mwandishi Wetu
Halmashauri Kuu ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini, kwa masikitiko makubwa inatangaza kifo cha Mchungaji Batare Kasongwa.
taarifa ya msiba huu imetolewa na Mch. Jairi Sengo – Makamu Mwenyekiti Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini, kwa niaba ya Halmashauri Kuu.
Ibada ya Mazishi ya mpendwa wetu Mchungaji Batare Kasongwa inatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 06/02/2025 Busale Moravian Wilaya ya Kusini (Kyela) kisha kufuatiwa na shughuli ya kumpunzisha katika nyumba yake ya milele.
“Pumzika kwa amani mpendwa wetu Mchungaji Batare Kasongwa”