

31 January 2025, 21:49
Kwenye maisha unapaswa kujifunza kwa watu waliofanikiwa kwani kufanya hivyo kuonaongeza uelewa na kukupa mafanikio katika kile unafanya.
Na Kelvin Lameck
Watumishi wanaofanya kazi katika taasisi za elimu zilizo chini ya kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la Kusini Magharabi wametakiwa kufanya kazi kwa ueledi ili kuhakikisha wanawafunza vijana waweze kujitegemea.
Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa kanisa la Moravian jimbo la kusini Magharibi Ndugu Israel Mwakilasa wakati wa tafrija ya kumuaga mtumishi Larissa Schmidiger aliyekuwa akifanya kazi chuo cha ufundi Moravian.
Nae Makamu Mwenyekiti wa kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la kusini Magharibi Mch.Asulumenye Mwahalende amewaomba watumishi waendelee kutangaza kanisa na taasisi zake popote wanapokwenda hatua itakayoleta ufanisi katika kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha ufundi Moraviani Erick Mwakasege amesema wamejifunza jambo kubwa kutoka kwa mtumishi Larissa ikiwemo uvumilivu na ushirikiano katika kazi.
Hata hivyo Larissa Schmidiger ameeleza kufurahishwa na mazingira ya Chuo cha ufundi Moraviani pamoja na ukarimu mkubwa aliofanyiwa na kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la kusini Magharibi.