Baraka FM

Jamii yaaswa kutunza mazingira kuepuka mmonyoko wa ardhi

22 January 2025, 16:35

Wadau wa mazingira mkoa wa Mbeya

Ulinzi wa mazingira ni wa kila mtu katika jamii na ili usalama wa jamii uwe mzuri jamii haina budii kutunza mazingira.

Na mwandishi wetu

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Ndg: Said Juma Madito amewataka Wadau wa Mazingira Tanzania(Mbeya) kuhakikisha Mpango wa usimamizi wa Mlima Kawetire unakidhi Mahitaji ya Wadau na kulinda Urithi wa asili na kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali zake.

Madito ameyasema hayo Leo katika Hotuba yake ya Ufunguzi katika Kikao Maalumu cha Warsha ya Wadau wa Mazingira iliyoandaliwa kwa kusudi la kupitia na Kutoa Maoni katika rasimu ya Mpango wa usimamizi wa mifumo ya ikolojia ya Mlima Kawetire chini ya Mradi wa kujenga Uwezo wa Kitaifa katika Kusimamia Sheria ya usimamizi wa Mazingira yaani( Enhancing National Capacity in the implementation of the environmental management Act).

Hata hivyo amesema hatua hii ya kupitia rasimu ni Mhimu sana kwasababu inahakikisha Mpango huo inakuwa wa kina, jumuishi na unaofaa kwa Mahitaji ya Jamii na Mazingira kama ambavyo ilibainishwa katika kipenvele Cha .radi wa EMA Namba 4.4 kinachohusu masuala ya tathimini ya mifumo ya Milima na vilimana.

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Ndg: Said Juma Madito

Kwa kuzingatia kifungu namba 58 Cha Sheria ya Mazingira sura 191 kinaielekeza NEMC kwa Kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa kubainisha vilima na Milima iliyo hatarini au imeharibiwa Mazingira yake na hivyo kuhatarisha Maisha ya binadamu na mfumo ikolojia kwa ujumla.

Kazi hii ya tathimini ya Mlima Kawetire ni muendelezo wa Kazi ya awali iliyofanyika Agosti 2024 iliyolenga Kupima Hali ya Mazingira ya Mlima huo ikiwa ni Pamoja na Kutathimini Hali ya mimea, wanyama, na vyanzo vya Maji,Kutathimini athali za Shughuli za binadamu kama Kilimo, ukataji Miti na uchimbaji Madini kwenye Mazingira ya Mlima.

Lakini pia matumizi ya Maji,kuni ardhi ya Kilimo na Kutathimini hatari za mmomonyoko wa Udongo, Maporomoko ya Ardhi au majanga ya asili yanayoweza Kutokea tena baada ya Maporomoko ya awali.

Warsha hii ya siku Mbili imejumuisha Wataalamu Kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira(NEMC) Ofisi ya makamu wa RAIS, Wakala wa Misitu Tanzania,Ofisi za Maji Bonde la Rukwa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya na Ofisi za Kata ambazo zinaguswa na Mlima Kawetire, Machifu wa Mbeyana asasi zisizo za kiserikali zinazotunza Mazingira, Wenyeviti wa Mitaa ya Itezi na Gombe.