Askofu Pangani aungana na wanawake wa Moravian kumuenzi mch.Luise Plock
18 January 2025, 08:01
Safari ya dunia ni fupi ambapo inamfanya kila mtu kutafakari namna ya kumpendeza Mungu ili kuwa na mwisho mwema.
Na Hobokela Lwinga
Askofu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Robert Pangani ameongoza na kushiriki ibada ya kuenzi na kukumbuka mchango wa mwanzilishi wa idara ya wanawake katika kanisa hilo marehemu mchungaji Luise Plock aliyefariki January 02,2025 nchini Ujerumani.
Kutokana na kanisa kutambua mchango mkubwa kwa mchungaji huyo kanisa kupitia idara ya wanawake kwa kushirikiana na majimbo yameandaa ibada ambayo imefanyika katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Jakaranda.
Mbali na Askofu Pangani viongozi wengine walioshiriki ibada hiyo ni katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Ndugu Israel Mwakilasa na baadhi ya makatibu wa idara ya wanawake kutoka majimbo mbalimbali ya kanisa la Moravian Tanzania.
Ikumbukwe kuwa mchungaji Luise Plock ndiye mwanzilishi wa idara ya wanawake jimbo la kusini na Jimbo la kusini magharibi, amefariki January 02,2025 na amezikwa January 17,2025 huko nchini Ujerumani.Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.