Baraka FM

Viongozi wa serikali, dini na waumini watakiwa kuishi kwa upendo, unyeyekevu

4 January 2025, 10:49

Askofu Kenan Panja wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini akifundisha katika semina ya neno la Mungu inayoendelea katika kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi ushirika wa Yeriko Mbalizi(picha na Hobokela Lwinga)

Mungu anahitaji watu wenye unyeyekevu wa moyo watu wanaompa nafasi katika maisha yote ya Kiroho na kimwili.

Na Hobokela Lwinga

Wakristo wametakiwa kuishi maisha ya unanyenyekevu na upendo kwa jamii kwani kufanya hivyo ni kuonyesha kazi ya Yesu aliyoliachia kanisa.

Wito huo umetolewa na Askofu Kenan Panja wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini akifundisha katika semina ya neno la Mungu inayoendelea katika kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi ushirika wa Yeriko Mbalizi.

Baadhi ya waumini wakifuatilia mafundisho yanayotolewa katika semina Yeriko Moravian (picha na Hobokela Lwinga)

Askofu Panja amesema maisha ya mkiristo yanapaswa kuendana na maisha ya Yesu Kristo aliyoyaishi ya upendo na unyeyekevu.

Aidha askofu Panja amesema ili uweze kukubalika kwa Mungu ni lazima uwe na moyo wa Toba kila wakati mbele za Mungu.

Timu ya kusifu na kuabudu ikiongoza ibada ya kumwabudu Mungu katika semina Yeriko Moravian (picha na Hobokela Lwinga)

Katika hatua nyingine Askofu huyo amewata viongozi na watu wanaojiandaa kwenda kugombea Katika uchaguzi ujao kuwa wanyenyenyekevu katika kuwatumikia wananchi wanao wapa nafasi.

Awali mchungaji wa ushirika wa Yeriko Paul Mwampamba ametumia fursa ya kuwaasa waumini wake kushika mafundisho wanayopewa kwani ni msingi bora wa maisha ya rohoni na mwilini.

Mchungaji wa ushirika wa Yeriko Paul Mwampamba(picha na Hobokela Lwinga)

Semina inayoendelea katika kanisa la Moravian ushirika wa Yeriko ni semina ya siku kumi na nne imeanza December 29,2024 na itahitimishwa January 12,2025.