Baraka FM

RC Homera awataka wazazi, walezi kuwalinda watoto

31 December 2024, 07:52

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera

Watoto ni taifa la kesho kila mtu anawajibu wa kumlinda mtoto kwa namna yoyote na kuhakikisha anakuwa salama.

Na Hobokela Lwinga

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera ameitaka jamii kuendelea kulinda na kuwathamini watoto ili
waweze kutimiza ndoto zao na kuisaidia jamii na Taifa kwa ujumla.

Homera ameeleza hayo wakati akikabidhi chakula kwa watoto yatima wanao lelewa kwenye vituo vya kulelea watoto, kilicho tolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa watoto hao kwaajili ya kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa 2025.

Homera amesema chakula hicho kitatolewa kwenye vituo sita vya kulelea watoto yatima ambapo kila kituo kitapata Mbuzi mbili, Michele kilo 20, Maharage kilo 20 na Mafuta Lita 10.

Nao baadhi ya wasimamizi wa vituo hivyo wameeleza umuhimu wa kupewa chakula hicho kwa watoto wao Huku mwakilishi wa watoto kutoka kituo cha Nuru jijini Mbeya akitoa shukurani kwa Rais Samia Suluhu Hassan.