Baraka FM

Wakristo watakiwa kuthamini ibada ya kumtolea Mungu sadaka

26 December 2024, 21:04

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi mch.Lawrance Nzowa(picha na Hobokela Lwinga)

Sadaka ni moja ya ibada ambayo inapewa nafasi kwenye maeneo mengi na zipo sadaka zinatolewa maeneo mbalimbali ikiwemo miungu,je ipi maana halisi ya sadaka kibiblia.

Na Hobokela Lwinga

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi mch.Lawrance Nzowa amewataka waumini kuthamini ibada ya kumtolea Mungu sadaka kwani kufanya hivyo ni kujiwekea hazina mbinguni na kumpenda Mungu.

Wito huo ameutoa wakati akiwasilisha salamu za jimbo wa waumini wa kanisa la Moravian ushirika wa Nsala uliopo Vwawa Mbozi mkoani Songwe.

Mchungaji Nzowa ametumia fursa hiyo kuwashukru waumini wa jimbo lake kwa kuendelea kuwa watoaji wa sadaka huku akisema sadaka ambazo wameendelea kutoa zimekuwa zikifanya kazi ya maendeleo ya kanisa.

Baadhi ya waumini wakiwa katika ibada ushirikani nsala (picha na Hobokela Lwinga)

Aidha mwenyekiti huyo amewataka waumini kuendelea kuliombea kanisa na taifa ili amani iendelee kudumu.

Akihubiri katika ibada hiyo mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania ushirika wa London Samwel Mwambene amesema kama wakristo wanapaswa kuishi maisha ya upendo kama kristo alivyoagiza kupitia Biblia.

mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania ushirika wa London Samwel Mwambene(picha na Hobokela Lwinga)

Ushirika wa Nsala ni miongoni mwa shirika zinazounda jimbo la Mbozi ambapo katika ushirika huo ndipo yanapatikana makao makuu ya jimbo Hilo.