

26 December 2024, 20:46
Katika maisha yoyote iwe ya kimwili au Kiroho yanahitaji uaminifu ili kuweza kufanikiwa.
Na Hobokela Lwinga
Askofu wa kanisa la Morovian Tanzania jimbo la mashariki Lawi Afwilile Mwankuga amewasisitiza viongozi wa dini kuwa na roho ya uaminifu wanapo kutana na mazingira magumu yanaweza kujaribu imani zao.
Kiongozi huyo wa dini ameyasema hayo leo katika ibada ya siku ya kukumbuka wafia imani ambayo imefanyika katika kanisa la kiinjili la kirutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Mbezi Beach jijini Dar es salaam.
Ameongeza kwa kuwataka viongozi hao kuwa imara katika kutetea imani aliyoiacha Yesu Kristo ili wawe mashahidi wake waaminifu kama utamaduni wa mitume wa Yesu.