Baraka FM

Waumini wametakiwa kutenda mema na kuacha uovu

25 December 2024, 13:06

Mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Chunya Godfrey Tinga(picha na Hobokela Lwinga)

Sherehe ya Kristmas kwa mkiristo ni kiashiria cha kukumbuka upendo wa Mungu kwa mwanadamu kwa ujio wa Yesu Kristo mkombozi wa ulimwengu.

Na Hobokela Lwinga

Wakristo duniani wametakiwa kutenda mema ili kuwa kielelezo kuonyesha kwamba ni wafuasi wa Mungu hali itakayo wafanya kuwavuta wengine kuwa wafuasi wa Mungu.

Baadhi ya washiriki wa ibada katika kanisa la Moravian ushirika wa Chunya Mbeya (picha na Hobokela Lwinga)

Wito huo umetolewa na mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Chunya Godfrey Tinga wakati akihubiri katika ibada ya Kristmas katika ushirika huo.

Mch.Tinga amesema wakristo wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kutokana na matendo yao wanayoishi.

Aidha mchungaji huyo amesema kipindi hiki ya sikukuu za jimbo mwisho wa mwaka kila mtu anapaswa kuonyesha upendo kwa watu wanaomzunguka.

Amesema maisha ya sasa yanahitaji Mungu apewe nafasi kwani hakuna mafanikio nje ya kumtengemea Mungu huku akiwataka kuacha kutegemea nguvu za giza.

Kwaya ya vijana kati (Paradise choir) wakiimba katika ibada ya Kristmas Chunya Moravian (picha na Hobokela Lwinga)

Katika hatua nyingine amewataka watu kukumbuka familia zao huku wakienda kutembelea maeneo waliyozaliwa kwa ajili ya kuhesabu kama ilivyoandikwa kwenye Bibilia.

Ibada hii imeambatana na huduma za ubatizo wa watoto na watu wazima,kurudi kundini na kupokea wakristo wanaohamia Moravian,na kipaimara.

Mchungaji Godfrey Tinga akitoa huduma ya mbaraka kwa wanafunzi wa kipaimara katika ibada ya Kristmas ushirika wa Chunya (picha na Hobokela Lwinga)