TAKUKURU Mbeya yafanya tathmini, mikakati ya chaguzi
23 December 2024, 18:09
Katika kupambana na vitendo vya Rushwa jamii imepaswa kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa pindi wanapoona vitendo hivyo.
Na Hobokela Lwinga
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Mbeya imefanya kongamano na wadau la thathimini ya uchaguzi serikali za mitaa 2024 na mkakati wa Kuzuia rushwa uchaguzi Mkuu 2025.
Kongamano hilo limefanyika katika makao makuu ya TAKUKURU mkoa wa Mbeya likiwa limehusisha viongozi wa dini, vyombo vya usafirishaji wa abiria na vyama vya siasa.
Akizungumza katika kongamano hilo Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya Maghela Ndimbo amesema jukumu la TAKUKURU ni kuzuia na kupambana na Rushwa.
Aidha amesema mapambano ya Rushwa yanahitaji ushirikiano na jamii kwa kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa.
Katika hatua nyingine ndimbo amesema katika uchaguzi ulipita hawajapokea taarifa yoyote ya vitendo vya Rushwa.
Nao viongozi wa dini wametoa mchango wao kuwa ni vyema viongozi wa vyama vya siasa kukemea vitendo vya rushwa kwenye vyama vyao.
Kwa upande wa viongozi wa vyama vya siasa wameiomba TAKUKURU kuendelea kutoa elimu kwa jamii huku wakiomba wale wote wanabainika na vitendo vya Rushwa wachukuliwe hatua za kisheria.