Baraka FM

Tume ya uchaguzi yaendelea kufanya mkutano na wadau wa uchaguzi

15 December 2024, 17:18

Baadhi ya viongozi wa tume ya uchaguzi(picha na Ezekiel Kamanga)

katika kuelekea uchaguzi mkuu viongozi wa tume ya uchaguzi wameendelea kufanya mikutano na wadau wa Uchaguzi katika maeneo mbalimbli hapa Nchini.

Na Ezekiel Kamanga

Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura umefanyika Jijini Mbeya mgeni rasmi akiwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Jacob Mwambegele lengo ni kupeana taarifa juu ya kuboresha daftari la mpiga kura.

Zoezi la maboresho nchini mpaka sasa limefanyika katika mikoa 21 na Mkoani Mbeya litafanyika kwa siku Saba kuanzia Disemba 27,2024 hadi Januari 2, 2025.

Viongozi wa tume ya uchaguzi pamoja na viongozi wa kidini na kimila(picha na Ezekiel Kamanga)

Mheshimiwa Jaji Jacob Mwambegele amesema kauli mbiu ya uchaguzi kuwa ni “Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora”.

Mkurugenzi wa uchaguzi Kailima Ramadhan Mkoani Mbeya jumla ya wapiga kura milioni moja wanatarajiwa kuandikishwa katika vituo elfu moja mia tano arobaini na saba.

Mkurugenzi wa uchaguzi Kailima Ramadhan Mkoani Mbeya(picha na Ezekiel Kamanga)

Aidha Kailima amesema baadhi ya Vituo ni Magereza ambapo wafungwa walio na kifungo chini ya miezi sita wataruhusiwa kujiandikisha na kupiga kura.

Katika hatua nyingine Kailima amesema watu watakaojiandolikisha mara mara mbili watakabiliwa na faini ya shilingi laki moja hadi laki tatu au kifungo cha cha miezi sita gerezani.

Akiahirisha mkutano huo mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Dkt Zakia Abubakary ameyashukuru makundi yote yaliyoshiriki sanjari na kutoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha daftari la npiga kura na kufanya maboresho kwa watu waliohamia maeneo mengine na kuhuisha taarifa zao.

Baadhi ya washiriki katika mkutano huo wakiwa Kwenye picha ya pamoja na viongozi wa tume ya uchaguzi (picha na Ezekiel Kamanga)

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo ni pamoja na Viongozi wa Kidini,Vyama vya Siasa,Asasi za Kiraia, Viongozi wa Kimila,Wahariri wa vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari.