Baraka FM

Free Pentecost Tanzania (FPCT) Jimbo la Mbeya lapata askofu mpya

5 December 2024, 20:27

Baadhi ya viongozi wakanisa la FPCT Mbeya(picha na Yuda Joseph)

Katika kuhakikisha huduma ya Mungu inafanyika kwa ubora na mwongozo mzuri lazima kuwepo na kiongozi wa kanisa, hivyo kanisa the Free Pentecost Tanzani (FPCT) Mbeya wamechagua Askofu wa jimbo hilo.

Na Yuda Joseph

Mkutano mkuu kupitia tume ya uchaguzi ya kanisa the free pentecost tanzani (FPCT) mbeya umemchagua mch Amos Igundu kuwa askofu mpya wa jimbo la Mbeya.

Mkutano huo umefanyika katika kanisa la FPCT jimbo kuu la mbeya forest ya kwanza jijini Mbeya.

Mwenyekiti wa tume amemtangaza Askofu Amos Igundu ndiye ataongoza kwa miaka mitano ijayo huku akiwashukuru wajumbe wa mkutano kwa ushirikiano walio utoa kukamilisha zoezi hilo

Viongozi waliochaguliwa wanna walio kaa mbele(picha na Yuda Joseph)
Sauti Mwenyekiti wa tume akitangaza matokeo

Aidha Mchungaji Amos Igundu baada ya kuchaguliwa ameomba ushirikiano kwa kwa wachungaji na waumini wote kwakipindi chote cha uongozi wake huku akihaidi kufanya kazi na watu wote.

Askofu aliye chaguliwa Mchungaji Amos Igundu(picha na Yuda Joseph)
Sauti ya Askofu Amos Igundu

katika mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe, ambo ni wapiga kura 103 ambao umewachagua viongozi wengine akiwemo Jacob Mwalisu kuwa msaidizi wa Askofu,Mchungaji Damson Ntangu kuwa mweka hazina akisaidiana sekelaga