Mwanaume auawa kwa kukatwakatwa, kupigwa mawe Mbeya
2 December 2024, 09:51
katika Hali isiyo ya kawaida mwili wa mtu umeokotwa mtaani akiwa amefariki.
Na Deus Mellah
Mtu mmoja jinsia ya kiume anaekadiliwa kuwa na umri wa miaka 22 Hadi 25 amekutwa ameuawa kwa kupigwa na mawe na mwili wake kukatwa katwa katika sehemu mbalimbali za mwili eneo la darajani njiapanda ya mapelele mtaa wa mwamfute kata ya ilemi.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa tukio hilo limeleta taharuki kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio Chans Mtikita amesema mwili wa mtu huyo umekatwa katwa kwa baadhi ya sehemu za mwili wake.
Naye mmoja wa aliyekuwa mgombea katika uchaguzi serikali za mtaa wa huo kwa tiketi ya chama che Democrasia Na Maendeleo CHADEMA Charles Kasyupa amesema Matukio Hayo Yamekuwa Ni Mengi Katika Kata Hiyo.
Pia mewataka wananchi wa eneo hilo kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake mtu anapobainika na kosa wamfikishe kwenye vyombo vya sheria.
Jitihada za kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya zinaendelea ili aweze kuthibitisha kutokea kwa tukio Hilo.