Baraka FM

Mchungaji Barthromeo Mahenge kanisa la Moravian afariki dunia

30 November 2024, 13:10

Marehemu mchungaji Barthromeo Mahenge

Duniani ni njia ambayo Kila aliyepewa pumzi ya kuishi na Mungu ni lazima apite na katika kulijua Hilo tunapaswa kujiandaa kimwili na kiroho kwa maisha yetu kuishi kwa kumpendeza Mungu ajuaye kesho ya Kila mtu maana yeye ndiye anayetoa na kutwaa.

Na Hobokela Lwinga

Mchungaji kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi mkoani Songwe Barthromeo Mahenge amefariki dunia usiku majira ya nne November 29,2024 katika hospitali inayomilikiwa na kanisa Hilo ya Mbozi mission alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo cha mchungaji Mahenge imetolewa na ofisi ya halmashauri kuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi kupitia kwa mwenyekiti wa Jimbo mch.Lawrance Nzowa.

Mwenyekiti kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi mch.Lawrance Nzowa.

Mchungaji Nzowa amesema marehemu Mahenge aliugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ambapo aligundulika kuwa na ugonjwa wa Typhoid pamoja na vidonda vya tumbo.

Aidha mchungaji Nzowa amesema enzi za uhai wa mchungaji Mahenge alitumika katika shirika mbalimbali na mpaka umauti unamfika alikuwa akitumika katika idara ya elimu ya kikristo katika wilaya ya Vwawa mtaa wa Ihanda katika kanisa la Moravian Jimbo la Mbozi.

Marehemu mchungaji Barthromeo Mahenge

Mchungaji Barthromeo Mahenge ameacha mke pamoja na watoto na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika mkoani Njombe siku ya Jumatatu December 02,2024.