TAKUKURU Mbeya yabaini deni la bilioni 4 kwenye mfuko wa NSSF
7 November 2024, 14:55
TAKUKURU Mbeya yashirikisha wananchi kuzuia vitendo vya rushwa kwenye miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 97.
Na Hobokela Lwinga
Taasisi ya ya kuzuia na kupamba na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Mbeya imefanya uchambuzi wa mifumo katika sekta ya hifadhi za jamii kwenye mfuko wa NSSF na kubaini uwepo wa madeni sugu ya michango ya wanachama kiasi cha shilingi bilioni 4 kwa baadhi ya waajiri kushindwa kuwasilisha kwenye mfuko huo.
Akitoa taarifa ya miezi mitatu julai hadi September 2024 kwa waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo Maghela Ndimbo amesema baada ya kubaini hali hiyo ilifanya kikao na waajiri na meneja wa NSSF mkoa wa Mbeya kukubaliana kumaliza changamoto zilizobainika ikiwemo kuwasilisha madeni hayo.
Aidha kamanda Ndimbo amesema Nyimbo amesema imebaini uwepo wa miradi miwili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 400 kuwa na mapungufu mbalimbali.
Kwa upande wa mashitaka TAKUKURU imeendesha mashauri 23 katika mahakama mbalimbali ndani ya mkoa wa Mbeya huku jamhuri ikishinda mashauri 8 kati ya 12 yaliyotolewa maamuzi.
Hata hivyo amesema katika Kipindi hicho wamewafikia wananchi na wadau mbalimbali 48,587 kwa kuwapatia elimu ya mapambano na kuzuia vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao ikiwa ni sambamba na uimarishwaji wa klabu za wapinga Rushwa.
Katika kuifikia adhima ya kutokomeza Rushwa nchini taasisi hiyo imekuwa na kauli mbiu isemayo kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu,tutimize wajibu wetu.