Askofu Mwakanani,waombeeni na kuwasaidia watu wenye uhitaji
5 November 2024, 11:48
Kutoa msaada kwa wahitaji hakutegemea cheo Wala hadhi ya mtu kila mtu inapaswa kumsaidia mahitaji yeyote mwenye uhitaji.
Na Kelvin Lameck
Waumini wa madhehebu mbalimbali nchini wametakiwa kuendelea kuwaombea na kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji wakiwemo yatima na walemavu.
Hayo yameelezwa na Askofu wa kanisa ya Brotherhood Tanzania lililopo Majengo jijini Mbeya Rabi Mwakanani wakati wa ibada maalumu iliyofanyika Novemba 3, 2024 kanisani hapo.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye Ulemavu mkoa wa Mbeya Damas Mwambeje amemshukuru Askofu Mwakanani na waumini wa kanisa hilo kwa kuwakarimu wahitaji na kwamba hiyo ni ibada njema mbele za Mungu.
Kwa upande wake Sister Kephania Mwambogolo kutoka kituo cha vijana walemavu Iyunga ameshukuru kanisa na watu wote waliojitoa kuwasaidia kwani misaada hiyo itasaidia kuwapunguzia ukali wa maisha.
Hata hivyo Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino mkoa wa Mbeya Cloud Mwakyoma ameiomba jamii kuwatendea mema watu wenye ulemavu kwani wana haki kama wengine.
Aidha mmoja wa waumini kanisani hapo Nyagi Bagoka amesema kuwa ibada hiyo ilikuwa nzuri kwa kuwa imegusa maisha ya watu kulingana na uhitaji waliokuwa nao.