Baraka FM

Askofu Pangani aonya waumini wanaofanya kampeni za uchaguzi kanisani

28 October 2024, 16:41

Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch.Robert Pangani(picha Hobokela Lwinga)

Kanisa linapaswa kutokuwa na kampeni za uchaguzi wakati wa uchaguzi wa viongozi.

Na Hobokela Lwinga

Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch.Robert Pangani ameonya watumishi wanaofanya kampeni ndani ya kanisa kuwa hatua hiyo inaweza kukwamisha kupata viongozi wazuri wa ngazi mbalimbali.

Askofu Pangani ameyasema hayo wakati akitoa salamu za Jimbo kwa waumini wa kanisa la Moravian ushirika wa Nzovwe jijini Mbeya.

Katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi akiwa ameongozana na mke wake katika ibada ushirikani Nzovwe (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch.Robert Pangani

Askofu Pangani amesema baadhi ya MAJIMBO katika kanisa la Moravian yameshindwa kupata maaskofu kutokana na kampeni ambazo zimekuwa zikifanywa na baadhi ya washiriki wa Mikutano ya Sinodi.

Aidha ametataja majimbo hayo kuwa ni Jimbo la ziwa Tanganyika (Kigoma) na Jimbo la kasikazini (Arusha) sambamba nakuwataka waumini kuendelea kuombea majimbo ambayo yanayotarajiwa kuwa na mikutano ya uchaguzi ikiwemo Jimbo la Mbozi.

Mchungaji Jonamu Msangawale wa Kanisa la Moravian ushirika wa Nzovwe Mbeya (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch.Robert Pangani

Katika Mkutano viongozi waliochaguliwa ni mchungaji Anorld Mbulwa kuwa mwenyekiti, mchungaji Abisai Jacob kuwa makamu mwenyekiti na mchungaji Damas Ndanda Bukika kuwa katibu mkuu.