Baraka FM

Moravian Kigoma yafanya uchaguzi wa viongozi

26 October 2024, 18:00

Hawa ndio viongozi waliochaguliwa na Mkutano mkuu Jimbo la ziwa Tanganyika

Demokrasia inapaswa kutumika mahali popote iwe kwenye taasisi za dini, binafsi au umma ili kupata lidhaa kutoka kwa watu wanaohitaji kuongozwa.

Na Hobokela Lwinga

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la lake Tanganyika(kigoma)limefanya mkutano mkuu wa Jimbo hilo na kuchagua viongozi mbalimbali ambao wataliongoza Jimbo kwa kipindi cha miaka mitano kwa mjibu wa katiba.

Katika Mkutano viongozi waliochaguliwa ni mchungaji Anorld Mbulwa kuwa mwenyekiti,mchungaji Abisai Jacob kuwa makamu mwenyekiti na mchungaji Damas Ndanda Bukika kuwa katibu mkuu.

Aidha katika sinodi hiyo uchaguzi wa kumpata askofu umeshindikana kutoka na dosari zilizojitokeza shirikani.

Katika mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kanisa la Moravian Tanzania na viongozi wa wengine wa majimbo yanayounda kanisa la Moravian Tanzania.